Thursday, December 04, 2014

MWANZA YAADHIMISHA SIKU YA WALEMAVU

             --Gwaride la vijana wakiandamana katika siku ya walemavu duniani

SHIRIKISHO LA WATU WENYE ULEEMAVU JIJINI MWANZA WAMEITAKA SERIKALI KUZIDISHA JITIHADA KATIKA KUPAMBANA NA CHANGAMANO ENDELEVU ZINAZOWAKABILI WALEMAVU NCHINI


HAYO YAMESEMWA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALEMAVU WILANI SENGEREMA BWN:JILIO NOCOLAUS  WAKATI AKISOMA RISALA YA SHIRIKISHO HILO MAPEMA JANA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU DUNIANI YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA GANDHALL JIJINI MWANZA

AIDHA KATIKA RISALA HIYO WALEMAVU WAMETOA MAPENDEKEZO YATAKAYOWAWEZESHA KWA USTAWI KATIKA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA MASUALA YA ELIMU AFYA USAFIRI NA UJASILIAMALI

                         -Baadhi ya walemavu wakionesha jumbe mbalimbali

AKIJIBU RISALA HIYO MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO HAYO AFISA USTAWI WA JAMII WA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA BI:EDITH NGOWI AMBAYE ALIMUWAKILISHA AFISA USTAWI WA JAMII  WA MKOA MWANZA AMESEMA SERIKALI INATAMBUA CHANGAMOTO ZA WALEMAVU NA INAENDELEA KUPAMBANA NAZO.
KWA UPANDE WAO BAADHI YA WALEMAVU WALIOHUDHURIA MAADHIMISHO HAYO WAKIZUNGUMZA NA KWA NEEMA FM RADIO WAMESEMA JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZAO BADO HAZIKIDHI
                         -Mgeni rasmi katika hafla hizo BI:EDITH NGOWI

SIKU YA WALEMAVU DUNIANI HUADHIMISHWA DEC 3 KILA MWAKA AMBAPO KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI MAENDELEO ENDELEVU AHADI NA TEKNOLOJIA IKILENGA KUWAWEZA WALEMAVU KATIKA TEKNOLOJIA
-Toka kushoto ni Jacktan msafiri mwandishi wa habari wa kwaneema fm akiwa na Salim Kikeke mwandishi wa BBC walihudhuria maadhimisho hayo.


NA: JACKTAN MSAFIRI

Monday, December 01, 2014

Askofu Kilaini na Nzigirwa Wafunguka Tuhuma Zinazowakabili

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini.

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.
Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni).

Akizungumza kwa simu jana, Askofu Kilaini alisema Rugemalira hupendelea kuchangia kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye peke yake aliyempatia mchango, bali kuna watu wengine wengi ambao wameshampatia na kazi yake ni kuipokea na kuifikisha sehemu husika.

Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake, simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena.

Hata hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na Gazeti la Mawio toleo la jana akisema fedha alizozipokea kutoka kwa Rugemalira ni kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kanisa Katoliki.

“Ndiyo nimepokea fedha kutoka kwa James na hii siyo mara ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya kijamii,” alisema Askofu Kilaini.

Alipotakiwa na gazeti hilo kuwataja wengine waliochangia kanisa lake na kama nao wamechanga kutoka kwenye fedha za akaunti ya escrow, alisema yeye hayumo kwenye michango hiyo.

Alipoulizwa anawezaje kusema hayumo kwenye orodha ya waliopewa fedha kutoka akaunti ya escrow wakati anakiri kuwa aliingiziwa mamilioni ya shilingi na Rugemalira, alisema michango inayoletwa kwake haina siri, hivyo wezi halisi ndiyo wakamatwe.

“Michango inayoletwa kwangu haina siri, shikeni wezi halisi,” alisema.

Askofu Nzigirwa
Kwa upande wake, Askofu Nzigirwa ambaye alirithi kiti cha Kilaini, cha Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam ameeleza kushtushwa kwake na ripoti ya PAC iliyomtaja yeye na Kilaini kuhusika katika uchotwaji wa Sh306 bilioni za escrow.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema anaandaa taarifa itakayofafanua kwa kina namna ambavyo fedha hizo zinazodaiwa zilitoka katika akaunti ya escrow zilivyoingizwa katika akaunti yake pamoja na hoja na maswali mengi yanayoulizwa na wananchi hasa waumini wa Katoliki kuhusiana na tuhuma hizo.
“Hizo taarifa zimenishtua sana. Bado nashangaa inakuwaje mimi naambiwa nimechota fedha kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow,” alisema Nzigirwa alipokuwa akizungumza na gazeti hili jana.

Nzigirwa alisema anachofahamu hadi sasa fedha zilizoingizwa katika akaunti yake hazihusiki na escrow lakini atafanya uchunguzi ili kupata undani wa fedha hizo na majibu yote yatakuwa katika taarifa atakayoitoa kwa vyombo vya habari siku yoyote kuanzia leo.

CDT...Mwananchi